Konta ajiaondoa katika michuano ya Charleston

Tenis Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mcheza tenisi Mwingereza Johanna Konta

Mcheza tenisi Mwingereza Johanna Konta amejiondoa katika mashindano ya tenisi ya wanawake ya Charleston yaliyoanza kutimua vumbi Jumatatu kutoka na kuwa na maumivu ya bega .

Konta mwenye umri wa miaka 25 alikua mwingereza wa kwanza kushinda taji la michuano ya wazi ya Miami kwa kumfunga Caroline Wozniacki jumamasi iliyopita.

Mchezaji huyo amesema "Michuano ya Charleston ni mashindano makubwa nilitarajia kushiriki lakini nilikua nikipambana na maumivu haya toka kwenye michuano ya Miami kuanzia mwanzo hadi mwisho

Mmarekani Madison Keys anayeshikilia nafasi ya 11 kwa ubora wa mchezo wa tenesi kwa wanawake duniani ndie mchezaji pekee anayesalia katika michezo hiyo akiwa na kiwango cha juu