Moyes kuhojiwa na Fa

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption David Moyes

Chama cha soka nchini England (Fa) kitamuhoji meneja wa Sundarland David Moyes baada ya kocha huyo kumwambia atampiga makofi mwandishi wa BBC Vicki Sparks.

Mwandishi huyo alimuuliza moyes uwepo wa mmiliki wa timu Ellis Short uwanjani unamletea wasiwasi wowote ndio kocha huyo akatoa maneno hayo ya vitisho.

Tukio hilo lilitokea tarehe 18 ya mwezi uliopita baada ya kumalizika mchezo wa wa ligi kuu England kati ya Sunderland na Burley .

Hata hivyo tayari David Moyes amekwisha muomba radhi mwandishi huyo na kujutia makosa yake.