Man united hali bado tete

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Phil Jagielka wa Everton akishangilia goli

Mashetani wekundu wa Manchester wamendelea na mwendo wa kukuasua katika ligi kuu ya England baada ya kuambulia sare ya goli 1-1 na Everton katika dimba la Old Traford.

Beki wa Everton Phil Jagielka ndie aliyeanza kuzifumania nyavu za Man United katika dakika ya 22, ya mchezo kabla ya Zlatan ibrahimovic kusawazisha goli hilo kwa mkwaju wa penati katika dakika za lala salama.

Leicester City wakicheza katika dimba lao la king power walichomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sunderland kwa mabao ya Islam Slimani na Jamie Vardy.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption mshambuliaji Jamie Vard akishangilia baada ya kuwafunga Sunderland

Wanajeshi wa wa njano wa Watford wakaibuka na ushindi wa mabao 2 - 0 dhidi ya West Bromwich, mabao ya Watford yakifungwa na Troy Deeney na Mbaye Niang.

Nao Burnley wakataka nyumbani kwa ushindi wa goli 1 - 0 dhidi ya Stoke City Jj