Mourinho: Luke Shaw alitumia mwili wake na ubongo wangu

Luke Shaw na Jose Mourinho Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Luke Shaw na Jose Mourinho

Meneja wa timu ya Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa Luke Shaw alitumia mwili wake lakini ubongo wa Mourinho wakati wa mechi kati ya Manchester United na Everton, ambayo ilisha kwa sare ya 1-1.

Shaw mwenye miaka 21, alicheza mara ya kwanza tangu Januari na ilikuwa penalty iliyotokana na mkwaju wake ambapo Zlatan Ibrahimovic alisawazisha.

"Alikuwa mbele yangu na nilikuwa nikimfanyia kila uamuzi" Mourninho alieleza

Shaw ndiye alikuwa mchezaji mdogo pekee kutoka Manchester aliyetengwa kando na Mourinho baada ya United ilitoka bao sare kwa mara ya tisa nyumbani katika ligi msimu huu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zlatan Ibrahimovic amefunga magoli 27 msimu huu

United ilimshukuru Ibrahimovic tena kwa penalty aliyoufunga iliyosaidia United kupata alama moja na kuiweka United nambari tano kwa jedwali.

Ibrahimovic ambaye mkataba wake unakamilika mwisho wa msimu huu bado hajaamua iwapo atasalia kubaki Old Trafford msimu ujao.

"Bado tunajadiliana, tungoje kuona matokeo, bado nipo wazi na hakuna lolote limetendeka bado", Ibrahimovic ambaye ana miaka 35 alieleza televisheni ya manchester united.

"Nilikuja hapa bila Ligi ya Mabingwa, haikuwa timu ambayo ilitarajiwa kushinda, lakini bado nilikuja na nikasaidia nilivyoweza ili kuiimarisha, kwa hivyo tungojee kuona matokeo.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Luke Shaw maecjhean Man U mara 16 pekee msimu huu