Guardiola: ''Hatukutosha msimu huu''

Mkufunzi wa Manchester City anasema kuwa timu yake haikutosha mboga msimu huu
Image caption Mkufunzi wa Manchester City anasema kuwa timu yake haikutosha mboga msimu huu

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amesema msimu wake wa kwanza katika ligi kuu ya Uingereza haujakuwa mzuri lakini ameahidi kuimarisha kikosi chake katika siku za usoni.

City iko katika nafasi ya nne katika ligi kufuatia kushindwa na Chelsea siku ya Jumatano, na hivyobasi kumaliza matumaini ya kocha huyo kushinda taji la ligi msimu wake wa kwanza katika ligi ya Uingereza.

''Katika siku zijazo nitajiimarisha'',alisema mkufunzi huyo wa zamani wa Bareclona na Bayern Munich.

''Msimu huu umekuwa funzo kubwa kwangu''.

Aliongezea: Tuna vitu vizuri kuwania na kufuzu katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.lakini lazima tuwe waaminifu.hatukuwa wazuri kuwania taji la ligi.

Kushindwa kwa City katika uwanja wa Stamford Bridge kumeiacha timu hiyo ikiwa mbele ya Arsenal na Manchester United kwa pointi nne huku timu zote mbili zikiwa na mechi moja kucheza.