Manchester United waitandika Sunderland 3-0

Manchester United waitandika Sunderland bao 3-0 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester United waitandika Sunderland bao 3-0

Matumaini ya Sunderland yamedidimia kwa mara nyingine baaada ya kutandikwa na Manchester United mabao 3-0.

Ushindi huo unaiwezesha Man U kupanda hadi nafasi ya tano katika jedwali.

Sunderland ilicheza na kikosi cha watu 10 baada ya Sebastian Larsson kupewa kadi nyekundi alipomchezea vibaya Ander Herrera.

Wakati huo Zlatan Ibrahimovic alikuwa taraia ameiweka Mancheter United kileleni kwa bao moja.

Henrikh Mkhitaryan aliifunga bao la pili huku naye Marcus Rashford akifunga bao la tatu.

Sunderland wanatafuta pointi 10 kujiokoa kutimuliwa kutoka ligi huku wakiwa na mechi 7 pekee za kucheza wakiwa hawajafunga goli katika mechi saba.

United, wamewapiku Arsenal wakiwa pointi nne nyuma ya Manchester City.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Manchester United waitandika Sunderland bao 3-0

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea