Kyrgios aing'arisha Australia Davies Cup

Nick Kyrgios alishinda pia mchezo wake wa mmoja mmoja dhidi ya Marekani
Image caption Nick Kyrgios alishinda pia mchezo wake wa mmoja mmoja dhidi ya Marekani

Nick Kyrgios ameiongoza vyema timu yake ya Australia kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Davies Cup baada ya kufanikiwa kuichapa Marekani.

Wameshinda kwa seti 7-6 (7-4) 6-3 6-4.

Australia iliyokuwa ikiongozwa na Lleyton Hewitt kwa sasa watavaana na timu ya Ubelgiji katika hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kuwachapa Italia siku ya jana Jumapili.

Image caption Nick Kyrgios amekuwa kwenye kiwango cha juu siku za hivi karibuni

Washindi mara tano wa michuano hiyo Uhispania walitolewa kirahisi na Serbia baada ya kurejea kwa mchezaji mahiri Novak Djokovic katika kikosi hicho.

Kwa upande wa Uingereza walishindwa kuendelea na mihuano hiyo baada ya kuchapwa na Ufaransa siku ya Jumapili.