Arsenal kucheza dhidi ya Crystal Palace ugenini

Emiliano Martinez Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kipa wa Arsenal Emiliano Martinez

Crystal Palace huenda ikawakosa hadi wachezaji 11 kutokana na majeraha lakini mchezaji anarudi baada ya mkewe kujifungua.

James McAurther hajulikani iwapo atashiriki mechi hiyo kutokana na jeraha la mgongo ,lakini Scott Dann, patrick van Aanholt na James Tomkins hawtoshiriki

Kipa Emiliano Martinez ataanzishwa katika goli la Arsenal kwa kuwa Petr Cech na David Ospina wanaugua majeraha ya nyonga na mgongo.

Kiungo wa kati Francis Coquelin anarudi baada ya kukosa mchi ya ushindi dhidi ya West ham kutokana na sababu za kibinafsi.

Laurent Kolscieny atakosa mechi yake ya pili akiwa na jeraha la nyuma ya goti lakini anatarajiwa kurudi hivi karibuni.