Arsenal walala 3-0 mbele ya Crystal Palace

Kipindi cha pili Arsenal hawakupiga shuti lililolenga lango la Palace
Image caption Kipindi cha pili Arsenal hawakupiga shuti lililolenga lango la Palace

Crystal Palace imeendelea kurudisha matumaini ya kusalia kwenye ligi kuu ya England baada ya kuichapa Arsenal ambayo nayo inahaha kuingia nafasi ya nne baada ya kukumbana na wakati mgumu.

Iwapo Arsenal itashindwa kuingia nafasi nne bora, itakuwa ni mara ya kwanza tokea imeanza kunolewa na Arsene Wenger mwaka 1996.

Palace wameshinda kwa magoli 3-0 katika mchezo uliokuwa wa kusisimua.

Image caption Sam Allardyce hana rekodi ya kushusha timu daraja

Palace walianza kuongoza kupitia kwa Andros Townsend kisha dakika chache baadaye Yohan Cabaye akapachika goli la pili.

Image caption Mashabiki wa Arsenal bado wanataka Wenger aondoke

Luka Milivojevic akaiandikia Palace goli la tatu kwa mkwaju wa penalti na kuifanya kuwa alama sita juu ya mstari wa kushuka daraja.

Katika kipindi cha pili Arsenal hawakuweza kupiga shuti lililolenga lango la Palace.

Image caption Tokea ajiunge na Arsenal mwaka 1996, Wenger hajawahi kumaliza nje ya nne bora

Baadhi ya mashabiki wa Arsenal waliosafiri kutoka London walibeba mabango yanayomtaka mfaransa huyo kuachia ngazi.

Image caption Palace kwa sasa wamejikusanyia alama 34

Arsenal ipo alama saba nyuma ya timu ya nne ambayo ni Manchester City ikiwa pia imesalia na michezo nane kabla ya ligi kumalizika.