Mabao matatu ya Adebayor yatetemesha

Emmanuel Adebayor alikaa njee miezi saba bila ya kujiunga na klabu yoyote baada ya kutoka Crystal Palace, kabla ya kujiunga na Basaksehir mwezi Januari

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Emmanuel Adebayor alikaa njee miezi saba bila ya kujiunga na klabu yoyote baada ya kutoka Crystal Palace, kabla ya kujiunga na Basaksehir mwezi Januari

Emmanuel Adebayor alifunga jumla ya mabao matatu huku Istanbul Basaksehir, ikiicharaza wapinzani wao Galatasaray katika ligi kuu nchini Uturuki.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal na Tottenham, alitikisa wavu mara mbili kabla ya mapumziko ya kwanza na kutinga bao la tatu kunako dakika ya 57, huku Mustafa Pektemek, akiongeza bao la nne.

Mabao matatu mfululizo ya Adebayor kwa mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2011 huko Real Madrid, huku sasa mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 33 akiwa amefunga jumla ya mabao 5, tangu alipojiunga na timu hiyo ya Basaksehir mwezi Januari mwaka huu.

Timu yake iko alama tano nyuma ya vinara Besiktas, huku wakisalia na mechi 8 tu msimu huu.