Kinara wa upinzani nchini Zambia azuia msafara wa Rais

Bw Hakainde Hichilema, ni kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zambia
Maelezo ya picha,

Bw Hakainde Hichilema, ni kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zambia

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema, alizuia msafara wa Rais wa nchi hiyo Edgar Lungu mwishoni mwa juma.

Hii ni kulingana na taarifa iliyotolewa kutoka kwa msemaji wa rais.

Amos Chanda, amesema kuwa msafara wa Bw Hichilema, iliendelea kudumisha njia yake ya kupitia magari barabarani, badala ya kuondoka barabarani ili kupisha msafara wa magari ya Rais kuweza kupita.

Haijafahamika iwapo hatua hiyo inatokana na kisa cha mara kwa mara cha kuvamia nyumba ya Bw Hichilema iliyoko katika mji mkuu, Lusaka.

Kwa sasa kiongozi huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi.

Ameliambia gazeti moja la Afrika Kusini- Daily Maverick kwamba, rais anataka kumuuwa.

Bw Hichilema, alipewa dhamana mwezi Oktoba mwaka jana, baada ya kushtakiwa kwa kosa la fitna, hatua ambayo kikosi chake kilisema ni mbinu za chama tawala za kutaka kumnyamazisha.