UEFA: Mlipuko wakumba basi la Borussia Dortmund nchini Ujerumani

Borussia Dortmund defender and Spain international Marc Bartra Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mchezaji wa Borussia Dortmund Marc Barta

Klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani imethibitisha kwamba mechi kati ya klabu hiyo na Monaco imeahirishwa.

Hii ni baada ya kutokea kwa mlipuko katika basi lililokuwa linasafirisha wachezaji wa klabu hiyo kwenda uwanjani.

Mechi hiyo ya robofainali katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya sasa itachezwa kesho.

Mchezaji wa Dortmund Marc Bartra amejeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.

Klabu hiyo imeandika kwenye Twitter kwamba wachezaji wengine wako salama na kwamba hakukuwa na hatari yoyote ndani au karibu na uwanja.

Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa vioo vya madirisha ya basi hilo vimevunjika kutokana na mlipuko huo.

Polisi katika jimbo la North-Rhine Westphalia wamefika eneo la tukio na kuanzisha uchunguzi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mashabiki wa Borussia Dortmund

Maafisa wa polisi wamesema kulitokea milipuko mitatu karibu na eneo la basi hilo.

Dortmund kwa sasa wanashikilia nafasi ya nne katika ligi kuu ya Ujerumani.

Mechi nyingine ya robofainali kati ya Barcelona na Juventus nchini Italia inaendelea.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ujumbe uwanjani kuhusu mlipuko huo

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii