UEFA: Barcelona yabamizwa na Juventus 3-0 Klabu Bingwa

Juventus Haki miliki ya picha Mike Hewitt
Image caption Juventus waliwapa kisago Barca

Barcelona imechabangwa magoli matatu kwa sufuri na Juventus katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.

Paulo Dybala alifunga magoli mawili katika dakika ya 7 na ya 22. Bao la tatu lilifungwa na Giorgio Chiellini katika dakika ya 55.

Barcelona walicheza kufa na kupona kujaribu kupata japo bao moja la ugenini lakini hawakuweza kufua dafu.

Image caption Juhudi za Messi na Neymar hazikufua dafu

Mchezo mwingine wa robo fainali kati ya Borussia Dortmund dhidi ya Monaco uliahirishwa baada ya basi ya Dortmund kushambuliwa.

Mchezo wa marudiano ni wiki ijayo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii