Bayern Munich kuchuana na Real Madrid

Carlo Ancelotti na Zinedine Zidane

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Carlo Ancelotti na Zinedine Zidane

Bayern Munich huenda ikacheza bila mshambuliaji Robert Lewandowski katika robo fainali ya mechi ya vilabu bingwa nyumbani dhidi ya Real Madrid.

Lewandowski ambaye amefunga mabao 38 katika mechi 40 msimu huu huenda asishiriki katika mechi hiyo kutokana na jeraha la bega.

Hatahivyo ,mkufunzi wa Bayern Carlo Ancelotti ambaye aliongoza Real Madrid kushinda taji lao la Ulaya kwa mara ya 10 mwaka 2014 anasema kuwa timu hiyo ya Ujerumani bado ni ngumu bila mshambuliaji huyo.

''Iwapo anahisi uchungu hatocheza ,lakini haitabadili mipango yetu'', alisema.

''Tutaamua iwapo Lewandowksi atacheza siku ya Jumatano.Tunajua umuhimu wake lakini haitabaili motisha wetu''.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Robert Lewandowski anaguza jeraha la bega

Anceloti anatarajia kwamba kipa Manuel Neuer atarudi baada ya kuuguza jeraha la mguu, lakini mlinzi Mats Hummel yuko nje baada ya kujiumiza mguu wakati timu hiyo ilipoicharaza Dortmund 4-1