Bayern Munich walala 2-1 mbele ya Real Madrid

Ronaldo anashikilia rekodi ya ufungaji muda wote barani Ulaya akiwa na magoli 100
Maelezo ya picha,

Ronaldo anashikilia rekodi ya ufungaji muda wote barani Ulaya akiwa na magoli 100

Cristiano Ronaldo amemaliza ukame wa miezi saba kwenye ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kuandika magoli mawili katika mchezo ambao Bayern Munich wamepoteza kwa magoli 2-1 dhidi ya Real Madrid.

Kwa sasa anafikisha magoli 100 na kuendelea kuwa kinara wa ufungaji Ulaya.

Maelezo ya picha,

Mlinda mlango Manuel Neuer alifanya kazi ya ziada katika mchezo huo

Arturo Vidal alipachika goli la kwanza lakini akakosa nafasi ya kuandika goli la pili baada ya kupaisha mkwaju wa penalti alioupiga.

Javi Martinez alilimwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu.

Bayern walitawaliwa baada ya kadi nyekundu na kujikuta muda mwingi wakiwa wanatafuta mpira.

Maelezo ya picha,

Mkwaju wa penalti wa Arturo Vidal ukipaa juu ya lango la Madrid

Mlinda mlango Manuel Neuer, aliokoa mikwaju ya hatari ikiwemo ya Gareth Bale, Karim Benzema na Ronaldo.