Manchester United yalazimishwa sare ya 1-1 na Anderlecht

Goli la Leander Dendoncker liliza matumaini ya Man U kuibuka na ushindi
Maelezo ya picha,

Goli la Leander Dendoncker liliza matumaini ya Man U kuibuka na ushindi

Manchester United wameshindwa kuondoka na ushindi ugenini dhidi ya Anderlecht baada ya kulazimishwa suluhu ya 1-1 katika hatua ya robo fainali.

Henrikh Mkhitaryan alianza kuiandikia bao United baada ya kazi nzuri ya Marcus Rashford Hii ikiwa ni dakika ya 37.

Kipindi cha kwanza Manchester United ikaenda mapumzikoni ikiwa kifua mbele kwa goli 1-0.

Maelezo ya picha,

Henrikh Mkhitaryan amefunga katika michuano minne mfululizo ya United ya ugenini

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikishambulia lango la mwenzake.

United ikiamini imemaliza kazi dakika ya 87 Leander Dendoncker akaiandikia Anderlecht goli la kusawazisha na kuhitimisha mchezo huo.

Marudio ya mchezo huu ni wiki ijayo na zamu hii United itakuwa nyumbani Old Trafford.