Tottenham yaikaribia Chelsea baada ya ushindi wa 4-0

Tottenham imeiadhabu Bounemouth 4-0
Maelezo ya picha,

Tottenham imeiadhabu Bounemouth 4-0

Tottenham imefanikiwa kushinda mechi 7 mfululizo za ligi ya Uingereza na kuendelea kuwakaribia viongozi wa ligi hiyo Chelsea baada ya kupata ushindi mzuri dhidi ya Bournemouth.

Tottenham ilinyakua ushindi huo katika dakika tatu za kipindi cha kwanza cha mechi baada ya Moussa Dembele kufunga bao la kwanza, Son Heung-min akapata la pili huku Harry Kane akifunga bao la tatu .

Bao hilo linamfanya mshambuliaji huyo wa miaka 23 kuwa mchezaji wa nne kufunga mabao 20 katika msimu mitatu ya Uingereza baada ya Alan Shearer, Ruud van Nistelrooy na Thiery Henry.

Vincent Janssen baadaye alifunga udhia baada ya kufunga bao lake la pili katika ligi ya Uingereza katika muda wa ziada ,dakika moja moja tu baada ya kuingia kama mchezaji wa ziada.