Liverpool yaizima West Brom 1-0 na kupanda ngazi

Roberto Firmino alifunga kwa kichwa Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Roberto Firmino alifunga kwa kichwa

Roberto Firmino alifunga bao la ushindi na kuiwezesha Liverpool kupanda hadi nafasi ya tatu katika jedwali la Primia Ligi

Mshambualia huyo mbrazil alifungia Liverpool mwisho mwisho ya kipindi cha kwanza.

Milner alifanya madhambi kipindi cha pilia lakiki Simon Mignolet, akafanikiwa kuukoa bao kutokana na mkwaju kutoka kwa Matt Phillips.

Baadaye Alberto Moreno akakosa la wazi baada ya kipa wa Albion Ben Foster kuruka kukoa kona.

Licha ya kukosa bao hilo kikosi cha Jurgen Klopp kilipata ushindi wa tatu katika mechi saba huku West Brom wakipata kipigo mara tatu mfululizo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Roberto Firmino na Philippe Coutinho wamefunga kati ya mabao 4 kati ya 5 ya Liverpool