Chelsea kuongoza bado licha ya kichapo

Marcus Rashford,akata utepe wa magoli dhidi ya Chelsea
Maelezo ya picha,

Marcus Rashford,akata utepe wa magoli dhidi ya Chelsea

Marcus Rashford dakika ya saba tu katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford anaifungulia Dimba Manchester United. Ander Herrera dakika ya 49 anaipa Manchester United bao la pili.

Pamoja na kufungwa, Chelsea inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 75 za mechi 32 wakati United inaendelea kushika nafasi ya tano kwa pointi 60 za mechi 31

Katika Mechi nyingine tunamshuhudia Roberto Firmino akiipatia Liverpool bao dhidi ya West Brom na hivyo Liverpool wanachupa sasa katika nafasi ya tatu ya Premier League.

West Brom wiki ijayo jumamosi watakutana na Leicester, Liverpool wakiwapokea Crystal Palace siku itakayofuata yaani jumapili.