Upendo wa wanariadha Kenya ulivyochipuka na kunawiri

Wakimbiaji wa Kenya, Paul Lonyangata na mkewe Purity walionyesha dunia jinsi wanavyopendana pale Paul alipopiga magoti na kumpatia mkewe maua baada ya wote kuibuka washindi wa Paris Marathon.

John Nene amezungumza nao mjini Eldoret katika bonde la ufa kutaka kujua zaidi kuhusu penzi lao.

Purity anatueleza ilimchukua muda Paul kabla ya afanikiwe licha ya ulimi wake mtamu.