Mashabiki wamrushia panya mchezaji nchini Denmark

Brondby ni wa pili katika Superliga

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Brondby ni wa pili katika Superliga

Mechi ya ligi kuu ya Denmark kati ya Brondby na FC Copenhagen ilitibuka baada ya mashabiki kuwarushia panya waliokufa uwanjani.

Mashabiki wa Brondby walimrushia panya mlinzi wa Copenhagen Ludwig Augustinsson alipokwenda kupiga kona.

Copenhagen ilishinda mechi hiyo 1 - 0 na sasa ni wa kwanza huku ikiishindia timu ya pili ambayo ni Brondby kwa alama 13.

"Sio vyema kuwa na baadhi ya wageni ambao hawawezi kuwa na tabia njema," alisema mkurugenzi wa michezo wa Brondby, Troels Bech.

Video iliyorekodi yaliyotokea uwanjani inaonyesha mchezaji wa Slovenia Benjamin Verbic akimsaidia mwenzake Augustinsson kuwatoa angalau panya wawili kutoka uwanja huo wa Brondby ambao unaweza kubeba mashabiki elfu 28.

Brondby ni mabingwa mara 10 wa Denmark na FC Copenhagen inayosimamiwa na aliyekuwa meneja wa Wolverhampton Wanderers Zamani Solbakken, wameweza kunyakua ushindi mara 11