Cristiano Ronaldo aandika historia kufikia magoli 100

Cristiano Ronaldo aandika historia kufikia magoli 100
Maelezo ya picha,

Cristiano Ronaldo aandika historia kufikia magoli 100

Cristiano Ronaldo ameandika historia ya kuwa mfungaji wa kwanza kufikia magoli 100 ya Champions League. Hatua hii ameifikia katika mechi ambayo pia amefunga hat-trick yaani magoli matatu ndani ya mechi iliyokamilika kwa Real Madrid kuwalaza Bayern Munich bao nne kwa tatu.

Rekodi hii ya Ronaldo inawatangulia Lionel Messi ambaye ana goli 94, Raul Gonzalez 71 na Ruud van Nistelrooy 56.

Hata hivyo mechi hii imezua malalamiko kadhaa ikiwamo Kadi nyekundu aliyoipigwa Vidal na pia inasemwa kuwa Ronaldo amefunga Goli la 'Off-side'.

Meneja wa Bayern Carlo Ancelotti amelalamika kwa kusema kuwa katika robo fainali kama hii unatakiwa kuwatumia waamuzi wazuri au ni wakati muafaka wa kuanzisha uamuzi kwa kutumia video, jambo ambalo UEFA wanalijaribu kwa kuwa kuna makosa mengi.

Katika mechi nyingine safari ya Leicester City ndiyo imekwamia hapo licha ya kutoka moja moja na Atletico Madrid. Leicester walikuwa wameutawala mchezo wakitengeneza nafasi nzuri kabisa lakini wakawekewa mlima mkubwa wa kupanda baada ya Saul Niguez dakika ya 26 kupiga kichwa kilichouelekeza mpira nyavuni.

Leo Mechi inayosubiriwa pale Camp Nou ni kati ya FC Barcelona na Juventus. Ikumbukwe Juve wana goli tatu kibindoni walizozibeba pale Turin.