UEFA: Leicester City watolewa Ligi ya Mabingwa na Atlético Madrid

Chanzo cha picha, Reuters
Saul Niguez's header was only the second home goal Leicester have conceded in the Champions League this season
Safari ya Leicester City katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu imefikia kikomo baada ya klabu hiyo ya Uingereza kutoka sare na Atletico Madrid uwanjani King Power.
Leicester waliondolewa katika hatua ya robofainali baada ya sare hiyo ya 1-1 kwani walikuwa wamelazwa 1-0 kwenye mechi ya mkondo wa kwanza.
Walitawala mechi hiyo katika uwanja huo wa nyumbani na wakaunda nafasi nyingi za kufunga.
Hata hivyo, walijipata wakiwa na mlima wa kukwea baada ya Saul Niguez kufunga bao kwa kichwa dakika ya 26.
Hilo lilikuwa na maana kwamba walihitaji angalau mabao matatu kipindi cha pili ili kufanikiwa kusonga.
Jamie Vardy alikomboa bao moja dakika ya 61 lakini Atletico walifanikiwa kujilinda hadi dakika ya mwisho na kuhakikisha wanajiunga na Real Madrid kwenye nusufainali.
Real waliwalaza Bayern Munich ya Ujerumani 4-2 na kupata ushindi wa jumla wa 6-1.
Chanzo cha picha, Rex Features
Atletico Madrid wamefungwa mabao matatu pekee mechi zao 10 walizocheza karibuni mashindano yote
Chanzo cha picha, Getty Images
Diego Godin aliondoa mpira eneo la hatari mara 17 mechi hiyo ya Jumanne