Man Utd kuchuana na Andaletch

Klabu hiyo inajiandaa wa robo fainali ya Europa League Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wayne Rooney nahodha wa Manchester United

Mechi za Europa League zinaingia kwenye mkondo wa pili wa robo fainali hii leo, huku Manchester United wakichuana na Anderlech katika uwanja wa Old Trafford.

Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney anarejea kwenye kikosi chake baada ya kuwa nje ya mechi nne kutokana na jeraha.

Meneja wa 'Man-U', Jose Mourinho amethibitisha kwamba mlinda lango Sergio Romero atakuwepo.

Rooney alifanya mazoezi na timu hapo Jumatano na Mourinho amesema alifurahishwa na mazoezi yake.

Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kuanza kipindi cha kwanza baada ya kusalia nje wakati wa mechi kati ya timu yake na Chelsea Jumapili iliyopita.

Manchester United wana matumaini ya kufika fainali za Europa hapo Mei 24.

Ikiwa Manchester United watashinda Europa League wataweza kupata nafasi katika michuano ya Klabu bingwa Ulaya hata kama watamaliza nje ya nne bora katika michuano ya ligi ya Uingereza.