UEFA: R. Madrid na A. Madrid, Monaco vs Juventus

Klabu ya Real Madrid iliposhinda taji la vilabu bingwa Ulaya
Image caption Klabu ya Real Madrid iliposhinda taji la vilabu bingwa Ulaya

Bingwa mtetezi wa kombe la vilabu bingwa Ulaya Real Madrid atakabiliana na wapinzani wao Atletico Madrid katika nusu fainali ya kombe la vilabu bingwa ikiwa ni marejeleo ya fainali ya mwaka jana.

Kikosi hicho cha Zinedine Zidane kitakuwa cha kwanza kulihifadhi taji hilo katika fainali mnamo tarehe 3 mwezi Juni huko Cardiff.

Klabu ya Ufaransa Monaco itakabiliana na klabu ya Juventus katika nusu fainali nyengine .

Awamu ya kwanza ya mechi hiyo itachezwa mnamo tarehe 2 na 3 Mei, huku awamu ya pili ikichezwa wiki itakayofuata.

Real ambayo inawania kushinda kwa mara ya 12 , iliwashinda mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich 6-3 kwa jumla ili kufuzu katika nusu fainali.

Atletico Madrid wakati huohuo ilisitisha matumaini ya klabu ya Leicester Ulaya, baada ya kuwashinda mabingwa hao wa Uingereza 2-1 katika awamu zote mbili.

Juventus ilipata ushindi wa 3-0 dhidi ya Bercelona huku Monaco ikiishinda Borussia Dortmund 6-3.