Chelsea kuchuana na Tottenham katika mechi ya FA

Harry Kane akitia wavuni bao dhidi ya Chelsea katika mechi ya awali
Image caption Harry Kane akitia wavuni bao dhidi ya Chelsea katika mechi ya awali

Mlinzi wa Chelsea Gary Cahill huenda asishiriki katika mechi ya nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Tottenham baada ya kutibiwa tatizo la tumbo, lakini Thibaut Courtois amepona jeraha la kifundo cha mguu ambalo lilimueka nje katika mechi dhidi ya Man United wikendi iliopita.

Marcos Alonso alikosa mechi hiyo baada ya kuuguza tumbo lakini haijulikani iwapo atarudi.

Kipa wa Spurs Hugo Lloris huenda akashiriki katika nusu fainali yake ya kwanza ya kombe la FA tangu 2014 kwa sababu Michel Vorm ambaye alikuwa amejiandaa kushiriki anauguza jeraha la goti.

Danny Rose amerudi katika mazoezi baada ya jeraha la goti lakini hatoshiriki.

Spurs imeshinda mechi 2 pekee kati ya mechi 16 dhidi ya Chelsea katika mashindano yote.

Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana katika kombe la FA 2012, Chelsea iliibuka mshindi kwa mabao 5-1 kabla ya kushinda ubingwa huo.

Mara ya mwisho kwa Tottenham kuibwaga Chelsea ilikuwa mwaka 1982 katika kombe la FA ambapo Spurs waliibuka na ushindi wa 3-2 katika raundi ya sita.