Chelsea yaivuruga Tottenham kombe la FA

Chelsea iliizaba Tottenham mabao 4-2 na hivyobasi kujikatia tiketi katika fainali ya kombe hilo dhidi ya mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Arsenal dhidi ya Manchester City. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Chelsea iliizaba Tottenham mabao 4-2 na hivyobasi kujikatia tiketi katika fainali ya kombe hilo dhidi ya mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Arsenal dhidi ya Manchester City.

Mchezaji wa Chelsea Nemanja Matic alifunga bao zuri kutoka mbali na kuisaidia timu yake kuinyamazisha Tottenham katika nusu fainali ya Kombe la FA katika uwanja wa Wembley.

Chelsea iliizaba Tottenham mabao 4-2 na hivyobasi kujikatia tiketi katika fainali ya kombe hilo dhidi ya mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Arsenal dhidi ya Manchester City.

Willlian aliiweka mbele Chelsea kunako dakika ya sita kwa kupiga mkwaju wa adhabu kabla ya kuongeza la pili kwa njia ya penalti kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.

Harry Kane alikuwa amesawazisha kutoka kwa krosi iliopigwa na Christian Ericksen kwa Suprs ambao walisawazisha tena kupitia bao la Delle Ali.

Mchezaji wa ziada Eden Hazard aliiweka Chelsea mbele kwa mara ya tatu kabla ya Matic kufunga bao la nne na kuiweka kifua mbele Chelsea.