Newcastle yarejea ligi kuu ya England

Newcastle Haki miliki ya picha PA
Image caption Ayoze Perez mfungaji wa mabao mawili ya Newcastle

Klabu ya Newcastle United msimu ujao watakipiga katika ligi kuu ya England ya baada ya kupanda tena daraja kutoka Championship kwa kuichapa timu ya Preston kwa mabao 4-1.

Mshambuliaji wa Newcaste Ayoze Perez ndie aliyeanza kuiandika timu yake goli la kuongoza katika dakika ya saba ya mchezo,Katika dakika ya kumi na nne Preston wakachomo goli hilo kupitia kwa mshambuliaji wake Jordan Hugill,

Kiungo Christian Atsu akaiongezea Newcastle bao la pili katika dakika ya arobaini na tano ya kipindi cha kwanza, katika dakika ya sitini na tano winga Matt Ritchie akaongeza bao la tatu kwa vijana wa Rafa Benitez kwa mkwaju wa penati.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wachezaji wa Newcastle wakishangilia ushindi

Mshambuliaji Ayoze Perez tena akashindilia msumari wa mwisho uliowahakishia Newcastle kurejea tena katika ligi kuu msimu ujao.