Arsenal kucheza dhidi ya leicester

Arsene Wenger akiishangilia timu yake baada ya kuibandua Manchester City katika kombe la FA Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsene Wenger akiishangilia timu yake baada ya kuibandua Manchester City katika kombe la FA

Mshambuliaji wa Arsenal Alex Oxlaide Chamberlain huenda akashiriki katika mechi dhidi ya Leicester City Licha ya kuondoka katika uwanja wa Wembley baada ya mechi ya Jumapili ya FA akiuguza jeraha.

Kiungo huyo wa kati aligongwa katika mguu lakini kcha Arsene Wenger anasema kuwa alichukua hatua ya tahadhari.

Mchezaji wa Leicester Wes Morgan anauguza jereha la mguu huku msimu wa Nampalys Mendy ukikamilika baada ya kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu.

Beki Robert Huth anarudi baada ya kuhudumia marufuku ya ligi ya klabu bingwa ,lakini Slimani anaendelea kuuguza jeraha.