Barca, Madrid zapeta La Liga

Barca Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Messi akifunga bao lake la 501 kwa Barcelona

Miamba ya soka la Hispania vilabu vya Barcelona na Real Madrid vimendelea kutamba katika ligi hiyo kwa kupata ushindi wa mabao mengi katika michezo yao.

Barcelona waliichapa timu inayoburuza mkia katika ligi Osasuna, kwa mabao 7 -1 mabao ya Barca yakifungwa na Lionel Messi aliyefunga mabao mawili, Andre Gomes, nae akafunga mawili kinda Francisco Alcacer, akatupia nae magoli mawili huku Javier Mascherano, akifunga bao moja.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption wachezaji wa Real Madrid wakipongezana

Real Madrid wakiwa ugenini katika dimba la Municipal de Riazor, waliwafunga Deportivo La Coruna, kwa mabao 6-2, mabao ya Real yalifungwa na James Rodriguez, aliyefunga mara mbili na mengine yakifungwa na Alvaro Morata, Lucas Vazquez, Isco na kiungo Casemiro

Leganes wakashinda kwa 3 - 0 dhidi ya Las Palmas, Nao Valencia wakalala nyumbani kwa kufungwa 3-2 na Real Sociedad.