Guardiola: Sijui kama Bravo atatuchezea tena

Claudio Bravo Haki miliki ya picha PA
Image caption Kipa wa Manchester City Claudio Bravo amekuwa na wakati mgumu England

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema hafahamu iwapo mlindalango wa klabu hiyo Claudio Bravo ataweza kucheza tena baada ya kuumia wakati wa mechi kati ya City na Manchester United Alhamisi.

Bravio, 34, aliondolewa uwanjani kwa machela baada ya kuumia akijaribu kuondosha mpira kutoka eneo la hatari wakati wa mechi hiyo ya Ligi ya Premia.

Willy Caballero aliingia nafasi yake.

"Bila shaka ni jeraha, labda litamuweka nje wiki kadha," alisema Guardiola,

"Sijui kama ataweza kucheza tena msimu huu."

Sare hiyo tasa, ambayo Bravo aliondoka uwanjani dakika ya 79, ilikuwa mechi yake ya sita kucheza kati ya 22 alizocheza Ligi ya Premia bila kufungwa tangu anunuliwe £15.4m kutoka Barcelona.

Mada zinazohusiana