Chelsea waunyuka Everton 3-0

Chelsea waunyuka Everton 3-0
Image caption Chelsea waunyuka Everton 3-0

Viongozi wa wa Ligi ya Premier Chelsea walipiga hatua kubwa kuelekea kushinda ligi baada ya kuwanyuka Everton mabao matatu kwa nunge.

Mabao yote ya Chelsea yalifungwa katika kipindi cha pili.

Ina maana kuwa hata kama Chelsea itashuka kwa pointi tatu kwenye mechi nne zilozosalia bado itachukua nafasi ya pili kwa miaka mitatu mfululizia hata kama Tottenham watashinda mechi zote zilizosalia.

Iliwalazimu Chelsea kusubiri kabla ya kombora ya Petro lililotumbukia wavuni mnamo dakika ya 66.

Everton walikuwa wameanza kwa kasi kwa mwendo wa kazi ambapo Dominic Lewin nusura afunge.

Sare ya Manchester City na Middlesbrough ina maana kuwaa klabu yake Ronald Koeman iko nyuma kwa pointi nane kutoka kwa klabu nne za kwanza huku ikibaki na mechi tatu tu.