Tottenham yailaza Arsenal

Haki miliki ya picha Google
Image caption Tottenham Hotspurs

Klabu ya soka ya Tottenham Hotspurs imefanikiwa kuwabwaga kwa bao 2-0 Arsenal kwenye Mechi ya Ligi Kuu England, iliyochezwa huko White Hart Lane ikiwa ni Dabi ya Jiji London Kaskazini.Magoli ya Tottenham katika mchezo huo yamefungwa na wachezaji Dele Alli pamoja na Harry Kane, kwa ushindi huo Hotspurs wamepaa hadi nafasi ya Pili wakiwa na alama 4 nyuma ya Vinara Chelsea, na kwa kichapo hicho Arsenal sasa wanashika nafasi ya 6 wakiwa nyuma ya Mananchester United ambao wao wamecheza dhidi ya Swansea city ambapo Manchester United walitoshana nguvu kufuatia sare ya kufungana bao 1-1.

Nao Midllesbra walitoshana nguvu na Manchester City kwa kufungana mabao 2-2.