Arsene Wenger aipongeza Tottenham

Haki miliki ya picha Google
Image caption Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amewapongeza Tottenham Hotspurs baada ya kushinda mchezo wao wa derby ya kaskazini mwa London katika Uwanja wa White Hart Lane kwa mabao ushindi wa bao 2-0 na kuwahakikishia nafasi ya kumaliza juu ya mahasimu wao kwa mara ya kwanza toka mwaka 1995.

Mabao ya Delle Alli na Harry Kane aliyefunga kwa penati yalitosha kuwahakikishia ushindi Spurs huku nafasi ya Arsenal wakimaliza kumaliza kwenye nafasi nne za juu .