Zlatan Ibrahimovic atarudi kucheza, wakala wake asema

Ibrahimovic hataweza kucheza mechi zilizosalia za msimu huu Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ibrahimovic hataweza kucheza mechi zilizosalia za msimu huu

Wakala wa mchezaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic, Mino Raiola, amesema mshambuliaji huyo amefanyiwa upasuaji kwenye goti lake na kwamba "atapona kabisa".

Amesema upasuaji huo ulifanikiwa.

Raia huyo wa Sweden mwenye miaka 35 aliumia kwenye kano za goti wakati wa mechi ya ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, dhidi ya Anderlecht mnamo 20 Aprili.

Lakini Raiola amesema kwenye taarifa kwamba jeraha alilopata mchezaji huyo halitishii uchezaji wake.

Ibrahimovic anakaribia kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja Old Trafford, na bado hajafikiana na klabu hiyo kuhusu mkataba mpya.

Amefunga mabao 28 msimu huu, baada ya kujiunga na United bila kulipiwa ada yoyote kutoka Paris St-Germain majira ya joto mwaka jana.

Tayari ameanza utaratibu wa kujiponya na kupata nafuu Pittsburgh.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii