Rekodi za riadha zilizowekwa kabla ya 2005 huenda zikafutwa

Svein Arne Hansen rais wa shirikisho la riadha Ulaya Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Svein Arne Hansen rais wa shirikisho la riadha Ulaya

Rekodi zote za dunia zilizowekwa na wanariadha kabla ya 2005 huenda zikafutiliwa mbali kufuatia pendekezo jipya kutoka kwa shirikisho la riadha barani Ulaya.

Uhalisi wa rekodi hizo uliangaziwa kufuatia kashfa za wanariadha kutumia dawa za kusisimua misuli .

Mwanariadha wa Uingereza Paula Radcliff ambaye anahofia kupoteza rekodi yake ya 2003 ametaja hatua hiyo kuwa ya uoga.

''Nimeumizwa na nahisi uharibifu huu huenda ukaniharibia sifa na heshima yangu'', alisema akiongozea kuwa shirikisho hilo la riadha limewafeli wanariadha wasafi.

Svein Arne Hansen ambaye ndio rais wa shirikisho la riadha barani Ulaya anasema kuwa rekodi za dunia zilizowekwa hazina maana yoyote iwapo watu hawana imani nazo.

Wanariadha wengi wa Afrika huenda wakaathiriwa iwapo pendekezo hilo la kuzifutilia mbali rekodi hizo litakubaliwa.

Shirikisho hilo la Ulaya limependekezo vigezo kadhaa ambavyo rekodi hizo zinafaa kutimiza.

-Rekodi hiyo iliafikiwa katika mashindano yaliopo katika orodha za michezo ya kimataifa ambapo viwango vya juu vya usimamizi na ufundi viliafikiwa.

-Iwapo mwanariadha huyo alikaguliwa miezi kadhaa kabla ya mashindano hayo.

-Iwapo sampuli za kupima dawa za kusisimua misuli zilichukuliwa baada ya kuvunja rekodi hiyo na zitatumiwa baada ya miaka 10.

-Kama rais wa shirikisho la riadha duniani IAAF ,Sebastian Coe anaunga mkono wazo hilo ili lifuatiliwe.

Huku ikiwa baadhi ya rekodi hizo hazivunjwi kila mara kama vile mita 1000, mita 2000, mita 20,000 na mita 30,000 zote zina rekodi zilizowekwa kulingana na mtandao wa IAAF.

Miongoni mwa watakaopteza rekodi zao ni pamoja na Hicham El Gerrouj na Kenenisa Bekele.

Rekodi za Afrika ambazo huenda zikafutwa:

Zilizowekwa nje:Outdoors

Noah Ngeny Kenya 1000m (Septemba 1999)

Hicham El Gerrouj Morocco 1500m (Julai 1998), maili moja (Julai 1999), 2000m (Septemba 1999)

Daniel Komen Kenya 3000m (Septemba 1996)

Kenenisa Bekele Ethiopia 5000m (Septemba 2004)

Tegla Loroupe Kenya 20,000m (Septemba 2000), 25,000m (Septemba 2002) 30,000m (Juni 2003)

Rekodi zilizowekwa ndani:

Frankie Fredericks Namibia 200m (Februari 1996)

Hicham El Grrrouj Morocco 1500m (Februari 1997), maili (Februari 1997)

Daniel Komen Kenya 3000m (Februari 1998)

Kenenisa Bekele Ethiopia 5000m (Februari 2004)