Zinedine Zidanne: Tumejiandaa dhidi ya Atletico Madrid

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidanne na mwenzake wa Atletico Diego Simone Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidanne na mwenzake wa Atletico Diego Simone

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema kuwa ushindi wa hapo awali dhidi ya Atletico Madrid hautakuwa na ushawishi wowote watakapokutana na Atletico Madrid wakati wa nusu fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Real Madrid iliishinda Atletico Madrid kwa njia ya penalti katika fainali za msimu uliopita na waliwashinda 4-1 katika msimu wa mwaka 2014.

''Ni mechi tofauti kabisa na watafanya kila kitu kuhakikisha kuwa wanafuzu'',alisema Zidanne.

Mshambuliaji wa Real Gareth Bale hatoshiriki mechi hiyo baada ya kupata jeraha la mguu huku naye mlinzi wa kulia wa Atletico Juanfran pia akikosekana kutokana na tatizo la paja.