Petra Kvitova aaanza kujifua

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Petra Kvitova

Mshindi wa mara mbili katika michuano ya Tenis ya Wimbledon Petra Kvitova amerejea katika mazoezi baada ya kuwa katika majeraha ya mkono wake wa kushoto.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alipata majeraha hayo ya mkono wakati akiwa nyumbani kwake Prostejov mnamo mwezi Desemba mwaka jana, ameweka picha yake katika mitandao ya kijamii akioneka anacheza kwa kufanya mazoezi akiwa mjini Monaco .