Aaron Lennon wa Everton augua ugonjwa wa kiakili

Aaron Lennon wa Everton augua tatizo la kiakili
Image caption Aaron Lennon wa Everton augua tatizo la kiakili

Winga wa klabu ya Everton Aaron Lennon amezuiliwa chini ya kifungu cha polisi cha afya ya kiakili kuhusu wasiwasi wa hali yake.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alipelekewa hospitalini kwa ukaguzi wa kiafya baada ya maafisa wa polisi kuitwa katika eneo la Salford siku ya Jumapili.

Lennon kwa sasa anapata matibabu kwa ugonjwa unaosababishwa na shinikizo la kiakili ,kulingana na klabu hiyo.

Mchezaji huyo wa Uingereza aliyejiunga na Everton kutoka Tottenham 2015 hajachezea kikosi cha kwanza tangu mwezi Januari.

Maafisa wa polisi wa Manchester walisema: Polisi waliitwa saa kumi na nusu mchana kufuatia wasiwasi wa mtu mmoja aliyekuwa katika barabara ya zamani ya eneo la Eccles .

Maafisa wa polisi waliitikia wito huo na mtu mwenye umri wa miaka 30 alikamatwa chini ya kifungu cha 136 cha afya ya kiakili na kupelekwa hositali kwa ukaguzi.

Habari kuhusu kulazwa kwa Lennon zilivutia ujumbe wa kumuombea katika mitandao ya kijamii miongoni mwa wachezaji wa soka na mashabiki wa klabu yake ya zamani na ya sasa.