Sulley Muntari apigwa marufuku ya mechi moja

Alipewa kadi ya manjano baada ya kumuomba refa asimamishe mechi akisemaalikuwa akibaguliwa kwa misingi ya rangi. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alipewa kadi ya manjano baada ya kumuomba refa asimamishe mechi akisemaalikuwa akibaguliwa kwa misingi ya rangi.

Kiungo wa kati wa Pascara Sulley Muntari, amepigwa marufuku ya mechi moja baada ya kulalamikia matamshi ya kibaguzi.

Alipewa kadi ya manjano baada ya kumuomba refa asimamishe mechi siku ya Jumapili dhidi ya Cagliari akisema kuwa alikuwa akibaguliwa kwa misingi ya rangi.

Mchezaji huyo wa zamani wa Ghana mweye umri wa miaka 32, kisha akaondoka uwanjani hatua iliyosababisha apewe kadi ya pili ya manjano.

Mafisa wamesema kuwa sio mashabiki wengi waliebdesha ubaguzi kuweza kuchukua hatua.

Kamati ya nidhamu ilikubaliana kuwa vitendo hivyo vilikuwa vibaya lakini sera zake haziruhu hatua kuchukuliwa kwa kuwa ni chini ya mashabiki 10 walihusika.

Sasa aliyekuwa mshabulijia wa Tottenham Garth Crook anasema kwa kila mchezaji wa kiafrika aliyeheshimiwa katika ligi ya Itaia, anahitaji kugoma wikendi hii iwapo Sulley Mitari hawezi kuondolewa marufuku ya kutocheza mechi moja.