UEFA: Juventus yawika ugenini yaichapa Monaco 2-0

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mchezaji Gonzalo Higuain

Klabu ya Juventus ya Italia imecheza ugenini usiku wa kuamkia leo dhidi ya FC Monaco katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali michuano ya Klabu bingwa ulaya na kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0 .

Mabao ya ushindi ya Juventus yalifungwa na Mchezaji Gonzalo Higuain katika dakika ya 29 kipindi cha kwanza na bao la pili Dakika ya 59 kipindi cha pili, na timu hizo zitarejeana tena mnamo mei 9 mwaka huu.

Image caption Klabu ya Juventus

Baada ya michezo miwili ya nusu fainali ya kuchezwa utafuta mchezo wa fainali utakaopigwa June 3 mjini Cardiff ukizikutanisha timu zilizofuzu hatua ya nusu fainali.