Ronald Koeman: Nitatumikia hadi mwisho mkataba Everton

Koeman alikuwa kocha msaidizi Barcelona 1998 hadi 2000 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Koeman alikuwa kocha msaidizi Barcelona 1998 hadi 2000

Meneja wa Everton Ronald Koeman amesisitiza kwamba atatumikia mkataba wake wa miaka mitatu hadi mwisho, licha ya kukiri kwamba angependa kuwa mkufunzi wa Barcelona siku moja.

Kwa sasa, anatumikia mwaka wa kwanza wa makataba wake Goodison Park, aliwasili huko akitokea Southampton mwaka jana.

Koeman, 54, aliambia gazeti la Sport la Catalonia kwamba angependa sana kuwa mkufunzi wa klabu yake ya zamani Barca.

Lakini Alhamisi, alisema: "Hakuna uwezekano kwamba nitaondoka Everton kabla ya kumaliza mkataba wangu."

Koeman amehusishwa na kurejea Nou Camp baada ya Luis Enrique kutanagza kwamba atang'atuka mwisho wa msimu.

"Sijioni nikiwa meneja wa Barca (atakayemrithi Enrique)," aliongeza.

"Nimetaja mara nyingi kwamba ni ndoto ya kila mwanadamu - kwa wachezaji, kwa mameneja. Hilo halibadilishi msimamo wangu au mkataba wangu Everton. Nina furaha sana, nasubiri kwa hamu msimu ujao."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Koeman alipokuwa anachezea Barca

Koeman alikaa miaka sita Barcelona akiwa beki kati ya 1989 na 1995.

Kwenye mahojiano na Sport, alikiri kwamba amejitolea kuhakikisha anafikisha Everton Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Mada zinazohusiana