Europa:Man U yang'aa ugenini yaifunga Celta Vigo 1-0

Image caption Mfungaji wa goli la Man U,Marcus Rashford,

Klabu ya soka ya Manchester United usiku wa kuamkia leo imechomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Celta Vigo katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Euefa Europa Ligi.

Goli pekee la Man U limewekwa kimiani na mshambuliaji kinda anayekuja kwa kasi Marcus Rashford mnamo dakika ya 67 kipindi cha pili cha mchezo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Manchester United yaibamiza Celta Vigo

Baada ya mchezo huo Timu hizo zitarejeana tena Alhamisi wiki ijayo huko Old Trafford Maskani ya Manchester United.