Epl-West Ham United kuivaa Tottenham

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption West Ham United kuivaa Tottenham

Ligi kuu ya soka ya England inatarajia kuendelea tena leo ijumaa kwa mchezo mmoja ambapo West Ham United wanawakaribisha Tottenham Hotspur.

West Ham United mpaka sasa wapo katika nafasi ya 15 katika msimamo ligi kwa alama 39, hivyo watahitaji kushinda mchezo huo ili kujikwamua kutuka nafasi hiyo kwenda nafasi ya tisa ,lakini pia Tottenham ingali wapo ugenini bila shaka watahitaji kushinda mchezo na kuwasogele kwa ukaribu vinara Chelsea.

Na kesho Jumamosi Manchester city watakuwa ni wenyeji wa Crystal Palace, Bournmouth watachuana na Stoke City,Burnley ni wenyeji wa West Brom,Hully city wanacheza na Sunderland, Leicester city watachuana na Watford na Swansea city watapepetana na Everton.