Sare yaisaidia Liverpool kuingia nafasi ya tatu

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Fraser Forster aliokoa penalti ya Milner

James Milner alikosa kufunga penalti kipindi cha pili na kuumbisha matumaini ya Liverpool kusalia katika kundi la timu nne za kwanza katika ligi ya Primia kufuatia sare na Southampton.

Kilikuwa kisa kilichowashangaza mashabiki ndaniaya Anfield.

"Bado kuna matumaini, tunachohitaji ni kucheza mechi zetu vyema." Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp alisema.

Fursa bora zaidi ya Liverpool ya kufunga bao ilikuwa dakika ya 66 wakati wakipata penalti baada ya Jack Stephens kumchezea vibaya Lucas.

Milner, ambaye hajawahi kosa kufunga penalti tangu mwaka 2009 alishuhudia mkwaju wake ukiokolewa na kipa wa Southampton.

Sasa sare hiyo itawasaidia Livepool kusonga hadi nafasi ya tatu mbele Manchester City

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Southampton