Mwanafunzi anayefanana na Lionel Messi nchini Iran azua gumzo

Iran Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Reza Parastesh kushoto na Lionel Messi kulia ,

Mwanafunzi mmoja nchini Iran amelazimika kupelekwa katika kituo cha polisi mwishoni mwa wiki iliyopita kisa na mkasa! Kufanana kulikokithiri na Lionel Messi.

Watu wengi katika mji wa Hamaden wamekuwa wakiomba kupiga picha na kijana huyo aitwaye Reza Parastesh, na hivyo kusababisha msongamano wa watu kila atakakokanyaga, hivyo polisi walilazimika kumhifadhi kwa muda ili kuondoa msongamano huo.

Mkanganyiko huo ulianza miezi michache iliyopita wakati ba a wa kijana huyo aliyefanana mno na Messi alipompiga picha akiwa amevalia fulana ya timu ya Barcelona yenye namba kumi.

Reza Parastesh, ana umri wa miaka ishirini na mitano kwa sasa, hivi karibuni alianzisha mtindo wa ukataji nywele na kupunguza ndevu zake mithili ya mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Argentina .

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Reza Parastesh akiwa katika picha na mabibi waliotaka ridhaa yake

Reza Parastesh, kwa sasa amebatizwa jina 'Messi wa Iran' amejikuta kila wakati na kila mahali akiombwa kupiga picha na watu wa aina kwa aina katika mji wa nyumbani kwao Hameden, nchini Iran.

Kijana huyo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kwa sasa watu watu wananiona mimi kuwa ndiye Messi wa Iran na kunitaka nifanye kiila kitu afanyacho Messi halisi, na pindi ninapotokeza mahali, watu hupatwa na mshtuko.

Nina furaha kubwa kuona kwamba ninawapa furaha na hili linapotokea linanipa ari mpya.

Parastesh aka Messi amekuwa ni mtu mwenye kufanyiwa mahojiano ya mara kwa mara na vituo vya habari na kufanikiwa kusaini mikataba mikubwa ya uoneshaji mavazi, na sasa ana fanya mazoezi makubwa ya kujua mbinu za mbira wa miguu ili akidhi vigezo wa Messi halisi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii