Rais wa Caf akataa kulipwa mshahara

Rais wa shirikisho la soka Afrika Ahmed amekataa kulipwa mshahara Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa shirikisho la soka Afrika Ahmed amekataa kulipwa mshahara

Rais wa shirikisho la soka barani Afrika Caf, Ahmed anasema kuwa amekataa kuchukua mshahara kutoka kwa shirikisho hilo.

Uchaguzi wake mnamo mwezi Machi ulimaliza uongozi wa miaka 29 wa aliyekuwa rais wa shirikisho hilo kutoka Cameroon Issa Hayatou.

''Nimekataa kuchukua mshahara kwa sababu sio heshima kwa usimamizi mzuri'', aliambia BBC Sport.

''Mishahara wa wafanyikazi wote wa Caf kutoka wasimamizi hadi maafisa wakuu na rais ni lazima iwe na uwazi''.

Raia huyo wa Madagascar mwenye umri wa miaka 57 alisimamia mkutano wake mkuu katika shirikisho hilo siku ya Jumatatu kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa shirikisho la Fifa siku ya Alhamisi.

Maswala muhimu yatakayozungumziwa ni namna ya kuifanyia mabadiliko Caf.

Tutachukua hatua ambayo itampendelea kila mtu ili kuhakikisha kwamba shindano hili linarudisha sifa yake na kuvutia raslimali mbali na ushaibiki mkubwa.

''Mabadiliko kuhusu usimamizi ni swala muhimu sana, kila mtu anapaswa kujua kinachotendeka'', alisema Ahmed.

Mada zinazohusiana