Fifa yaidhinisha nafasi mpya za Afrika Kombe la Dunia

Kuwepo kwa timu 48 ilikua ni moja ya ahadi ya Gianni Infantino katika kampeni zake
Image caption Kuwepo kwa timu 48 ilikua ni moja ya ahadi ya Gianni Infantino katika kampeni zake

Baraza la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeidhinisha uamuzi wa kulipatia bara la Afrika nafasi tisa timu zinazoshiriki fainali za Kombe la Dunia zitakapoongezwa na kuwa 48 mwaka 2026.

Hatua hiyo iliidhinishwa Jumatano nchini Bahrain.

Bara la Afrika kwa sasa huwa na nafasi tano pekee.

Taifa la kumi kutoka Afrika litashiriki katika michuano ya muondoano ya kufuzu, itakayoshirikisha nchi sita, kuamua atakayefaidi kutokana na nafasi mbili za ziada.

Baraza la Fifa lilitangaza pendekezo lake la kwanza kuhusu mpango wa kugawa nafasi hizo 48 tarehe 30 Machi.

Image caption Hatua ya nyongeza ya timu hizo inatajwa kama sababu mojawapo ya kuonekana kwa nchi ambazo zilikuwa hazipati nafasi

Nafasi mpya zitajazwa vipi?

Afrika - 9 kutoka timu za awali 5

Asia - 8 kutoka timu 4 za awali

Ulaya - 16 kutoka timu 13 za awali

Marekani ya Kaskazini, Kati na Caribbean - 6 kutoka timu 4 za awali

Bara la Oceania - 1 kutoka timu 1 ya awali

Amerika ya Kaskazini - 6 kutoka timu 4 za awali

Historia ya Mabadiliko Kombe la Dunia

Kombe la Dunia Timu
1930 Uruguay 13
1934 Italia 16
1950 Brazil 13
1954 Uswizi 16
1958 Sweden 16
1974 Ujerumani Magharibi 16
1982 Uhispania 24
1986 Mexico 24
1998 Ufaransa 32

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii