Arsenal yashinda na kupanda juu ya Manchester United

Alexi Sanchez aliifungia Arsenal bao la kwanza
Image caption Alexi Sanchez aliifungia Arsenal bao la kwanza

Arsenal imeimarisha matumaini yao ya kutaka kuwa katika timu nne bora katika jedwali la Uingereza kufuatia ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi ya Southampton.

Mabao hayo yalifungwa na Alexi Sanchez na Olivier Giroud.

Baada ya kipindi cha kwanza kilichokosa mchezo mzuri Sanchez aliwashangaza wengi baada ya kuwachenga walinzi wa Southampton na kisha kucheka na wavu.

Mchezaji wa ziada Giroud ambaye aliingia mahala pake Wellbeck aliimarisha ushindi huo kwa kufunga kwa kichwa muda mfupi baada ya kuingia uwanjani.

Southampton hawakufanya mashambulizi mengi katika safu ya ulinzi ya Arsenal.

Fursa yao kuu ilikuwa katika kipindi cha kwanza wakati Manolo Gabbiadini alipopiga mkwaju uliookolewa na Petr Cech.

Ushindi huo unamaanisha kwamba Arsenal inapanda juu ya Manchester United katika nafasi ya 5 ,alama tatu nyuma ya Manchester City.

Mada zinazohusiana