Afrika yapewa nafasi 9 kombe la dunia 2026

Yaya Toure anayeichezea Manchester City ameshiriki katika kila mechi ambayo Ivory Coast imecheza katika michuano mitatau ya kombe la dunia
Image caption Yaya Toure anayeichezea Manchester City ameshiriki katika kila mechi ambayo Ivory Coast imecheza katika michuano mitatau ya kombe la dunia

Baraza la shirikisho la soka duniani Fifa limeidhinisha mpango wa kulipatia bara la Afrika nafasi 9 wakati kombe la dunia litakapoongeza timu zitakazoshiriki katika kinyanganyiro hicho na kufikia 48, 2026.

Hatua hiyo ilithibitishwa siku ya Jumanne mjini Bahrain. Kwa sasa bara hilo lina nafasi 5 pekee.

Taifa la kumi la Afrika litashiriki katika mchuano wa muondoano utakaojumuisha mataifa sita ili kuamua kuhusu nafasi mbili.

Baraza la Fifa lilipendekeza vile litakavyotoa nafasi hizo 48 mnamo tarehe 30 mwezi Machi.

Kinyang'anyiro hicho kipya kitashirikisha timu 16 kutoka Ulaya.

Wanachama wa Fifa walipiga kura mnamo mwezi Januari kuongeza timu zitakazoshiriki kutoka 32 hadi 48 kuanzia dimba la mwaka 2026.

Mada zinazohusiana